IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
Idara ya Ardhi na Maliasili ni miongoni mwa Idara kubwa zilizopo katika Halmashauri ya Tarime. Idara hii imegawanyika katika vitengo vikubwa viwili (2) ambavyo ni Kitengo cha Ardhi na Kitengo cha Maliasili.
KITENGO CHA ARDHI:
Kitengo hiki kinahusika hasa na masuala yote yahusuyo ardhi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na Usimamizi wa ardhi, Umilikishaji na udhibiti wa matumizi ya ardhi, Upangaji wa Miji na Vijiji, Upimaji wa ardhi na uthamini. Ni sehemu inayolinda haki, wajibu na maslahi katika ardhi kwa kusimamia sheria, sera na kanuni zinazolinda maslahi katika ardhi. Kitengo hiki pia kinaundwa na vitengo vidogo vinne (4) ambavyo ni Kitengo kidogo cha Mipango Miji, Usimamizi wa Ardhi, Uthamini pamoja na Upimaji na Ramani.
Kitengo hiki kimegawanyika katika vitengo vidogo viwili (2) ambavyo ni Kitengo kidogo cha Misitu na Wanyamapori ambazo zinahusika na usimamizi na utunzaji wa maliasili zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Ni kitengo kinachowajibika katika usimamizi wa rasilimali za misitu na Wanyamapori katika halmashauri yetu yenye changamoto nyingi za uvamizi wa tembo na ujangili hasa katika vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kupitia kada ya Wanyamapori idara ina jukumu pia la kufanya doria na kudhibiti nyara za serikali, kusimamia na kutekeleza sheria Na. 5 ya Wanyama pori ya Mwaka 2009 pamoja na kusimamia shughuli za utalii.
Na |
KADA ZA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI |
IDADI YA WATUMISHI |
1 |
UTHAMINI
|
3 |
2 |
USIMAMIZI WA ARDHI
|
3 |
3 |
UPIMAJI NA RAMANI
|
5 |
4 |
MIPANGO MIJI
|
2 |
5 |
MISITU
|
3 |
6 |
WANYAMAPORI
|
7 |
JUMLA |
23 |
SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI.
KITENGO KIDOGO CHA MIPANGO MIJI.
Majukumu ya kazi za kila siku za kitengo kidogo cha mipango miji:-
KITENGO KIDOGO CHA UTHAMINI.
Majukumu ya kazi za kila siku za Kitengo kidogo cha Uthamini:-
KITENGO KIDOGO CHA USIMAMIZI WA ARDHI.
Majukumu ya kazi za kila siku za kitengo kidogo cha Usimamizi wa ardhi:-
KITENGO KIDOGO CHA UPIMAJI NA RAMANI.
Majukumu ya kazi za kila siku za kitengo kidogo cha Upimaji na ramani:-
KITENGO KIDOGO CHA MISITU.
Majukumu ya kazi za kila siku za kitengo kidogo cha Misitu:-
KITENGO KIDOGO CHA WANYAMAPORI.
Majukumu ya kazi za kila siku za kitengo kidogo cha Wanyamapori:-
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa