IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Idara ya Elimu ya Sekondari ni idara mpya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa iliyoanzishwa rasmi Julai 2009, baada ya agizo la Mhe. Rais la mwaka 2008 alipokuwa anatangaza Baraza la Mawaziri. Kabla ya hapo Idara hii ilikuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Idara hii ina majukumu mbalimbali, baadhi ya majukumu hayo ni:-
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuma jumla shule za sekondari 31 kati ya hizi, 29 ni za Serikali, 02 zinamilikiwa na taasisi za kidini. Aidha, kati ya shule 31 zilizopo katika Wilaya ya Tarime shule 03 zina kidato cha tano na sita ikiwa zote ni za Serikali.
Idara ya Elimu Sekondari inaundwa na vitengo viwili katika kutekeleza majukumu yake. Vitengo hivi ni kama ifuatavyo:-
IDADI YA WALIMU
Idara ya Elimu Sekondari ina jumla ya walimu 433 ikiwa walimu 338 ni wa Kiume na 95 wakiwa wa kike. Hata hivyo kati ya walimu hao 433, walimu 99 tu ndio wanaofundisha masomo ya Sayansi.
IDADI YA WANAFUNZI
Idara ya Elimu Sekondari inawanafunzi wapatao 10,259 ikiwa wavulana 6,171 na wasichana 4,088.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa