• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Mail za Ofisi |
    • Malalamiko |
TARIME DISTRICT COUNCIL
TARIME DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi na Awali
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Maendeleo ya Jamii,
      • Mipango na Uratibu
    • Kitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Shughuli za Kilimo
    • Shughuli za Ufugaji
    • Shughuli za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha, Mipango & Utawala
      • Elimu, Afya & Maji
      • Mazingira, Ujenzi & Uchumi
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Taratibu Mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za Shughuli Mbalimbali
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

JUKWAA LA WANAWAKE LAZINDULIWA TARIME.

Tuma: July 18th, 2017

Wanawake Wilayani Tarime wametakiwa kuondokana na dhana kuwa mwanamke anaweza akiwezeshwa kwani kauli hiyo huwafanya baadhi ya wanawake kushindwa kufanya shughuli mbalimali za maendeleo kwa imani kuwa bila kusaidiwa hawawezi kufanya kazi.

Hayo yalielezwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime Bw. John Marwa kwenye kikao cha uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Wilaya Tarime.

Marwa alisema kuwa wanawake wa Tarime ni wachapakazi wa maendeleo katika shughuli za ujasiliamali zikiwemo biashara za ndizi mbivu, viazi kwa kutumia mitaji yao wenyewe.

“Wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa ukiangalia hapa Tarime uchumi mkubwa unachangiwa na wanawake hususani biashara za ujasiliamali, katika soko la Rebu wanawake wanafanya biashara hivyo nawaomba wanawake Jukwaa hili linaloundwa liwe chachu katika shughuli za uzalishaji” alisema Katibu Tawala.

 Nae Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya Tarime Bw. Victor Kabuje alisema malengo ya jukwaa hilo ni kuwakutanisha wanawake ili kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za maendeleo.

“Lengo lingine ni kuongeza uelewa wa wanawake katika biashara, upatikanaji wa mitaji, sheria za nchi katika masuala ya uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi” alisema Kabuje.

Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Mara Bi. Noela Gachuma alisema sasa ni wakati wa wanawake kujikuza kibiashara kusaidia masuala ya uhabarishaji wa maeneo ambayo yanasaidia kuboresha biashara na shughuli za kiuchumi.

Katika kikao hicho wanawake walifanya uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la Wanawake, nafasi ya Mwenyekiti ilinyakuliwa na Bi. Mariam Mkono ambaye ni Diwani viti maalum kata ya Nyamwaga (CCM), Makamu Mwenyekiti Bi. Veronica Merengo na Katibu Bi. Mary Ntarisa wakiwa ni Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

18 Julai 2017.

Matangazo ya Kawaida

  • ORODHA YA VITAMBULISHO VYA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU March 20, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA (DAFTARI LA WAPIGA KURA). April 19, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA February 25, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZIYA MKATABA KWA MADEREVA. May 30, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI

    February 20, 2025
  • TANZIA

    March 15, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MARA ATEMBELEA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME

    February 26, 2025
  • MHE. EVANCE MTAMBI AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MWEMA NA RWGICHERI JUU YA CHANGAMOTO YA ARDHI

    February 24, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Maadhimisho ya Nanenane, 2024
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • eMrejesho
  • Dirisha la Watumishi
  • Taarifa za Mishahara
  • NeST-Mfumo wa kielektroni wa manunuzi Tanzania
  • Mfumo wa Usajili Mali iliyopotea
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa wafanyabiashara wadogowadogo
  • Mfumo wa Kibali cha kusafiri nje ya nchi
  • STAFF ASSESSMENT

Viungio Vinavyoshabiana

  • Government portal
  • TAMISEMI
  • HALMASHAURI WILAYA TARIME.BLOG
  • Magazeti mbalimbali
  • Jarida la Tarimedc
  • MWALIMU WETU MITIHANI MBALIMBALI

Idadi ya waliotembelea tovuti kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa