• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Mail za Ofisi |
    • Malalamiko |
TARIME DISTRICT COUNCIL
TARIME DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi na Awali
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Maendeleo ya Jamii,
      • Mipango na Uratibu
    • Kitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Shughuli za Kilimo
    • Shughuli za Ufugaji
    • Shughuli za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha, Mipango & Utawala
      • Elimu, Afya & Maji
      • Mazingira, Ujenzi & Uchumi
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Taratibu Mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za Shughuli Mbalimbali
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

KATIBU TAWALA TARIME AZINDUA CHANJO YA MINYOO NA KICHOCHO.

Tuma: July 19th, 2017

Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime Bw. John Marwa amesema ili mtoto  asome vizuri anahitaji kupata afya njema ikiwa ni pamoja na kupata chanjo ya minyoo, kichocho na magonjwa mengineyo.

Marwa ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa zoezi la chanjo ya Minyoo na Kichocho lililofanyika Kiwilaya katika Shule ya Msingi Nyamwaga ambapo aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime  Mhe. Moses Misiwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Apoo Castro Tindwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Boniventure Bisulu.

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  Amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani imetoa chanjo hiyo bure bila malipo yoyote na kwamba dawa hizo hazina madhara yoyote kwa matumizi ya binadamu. Hivyo wazazi waachane na dhana potofu ya kwamba watoto watazimia pindi wakitumia dawa.

Mwenyekiti wa Halmashauri alisisitiza suala  zima la kuzingatia sheria ya mtoto na kwamba kila mzazi anawajibu  wa kulinda afya ya mtoto na kuhakikisha mtoto anakuwa salama wakati wote.

Aliongeza kwa kuipongeza Serikali kwa kutoa chanjo hizo kwa watoto kwani itawakinga na magonjwa yanayoweza kuwasababishia kuwa na afya dhoofu.

Bw. Apoo aliishukuru pia serikali kwa kutoa chanjo na kuwasisitiza wazazi na watoto kuzingatia usafi wa mwili kwa ujumla. Alisema ili kujikinga na magonjwa ya minyoo ni muhimu kuzingatia usafi wa mazingira yanayotuzunguka na kutumia vyoo, pia kujenga desturi ya kupima afya zetu mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

Nae Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Boniventure Bisulu alifafanua kwamba Tanzania imeungana na Nchi nyingine katika kupiga vita Magonjwa yaliyosahaulika kama vile Kichocho na Minyoo na kwamba mpaka sasa inakadiriwa watu bilioni 2 wameathirika na Ugonjwa wa Kichocho.

Halmashari ya Wilaya Tarime inategemea kutoa chanjo kwa watoto 99,000 walio na umri kuanzia miaka 5 hadi 15.

 Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

19 Julai 2017.

Matangazo ya Kawaida

  • ORODHA YA VITAMBULISHO VYA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU March 20, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA (DAFTARI LA WAPIGA KURA). April 19, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA February 25, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZIYA MKATABA KWA MADEREVA. May 30, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI

    February 20, 2025
  • TANZIA

    March 15, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MARA ATEMBELEA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME

    February 26, 2025
  • MHE. EVANCE MTAMBI AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MWEMA NA RWGICHERI JUU YA CHANGAMOTO YA ARDHI

    February 24, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Maadhimisho ya Nanenane, 2024
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • eMrejesho
  • Dirisha la Watumishi
  • Taarifa za Mishahara
  • NeST-Mfumo wa kielektroni wa manunuzi Tanzania
  • Mfumo wa Usajili Mali iliyopotea
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa wafanyabiashara wadogowadogo
  • Mfumo wa Kibali cha kusafiri nje ya nchi
  • STAFF ASSESSMENT

Viungio Vinavyoshabiana

  • Government portal
  • TAMISEMI
  • HALMASHAURI WILAYA TARIME.BLOG
  • Magazeti mbalimbali
  • Jarida la Tarimedc
  • MWALIMU WETU MITIHANI MBALIMBALI

Idadi ya waliotembelea tovuti kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa