• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Mail za Ofisi |
    • Malalamiko |
TARIME DISTRICT COUNCIL
TARIME DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi na Awali
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Maendeleo ya Jamii,
      • Mipango na Uratibu
    • Kitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Shughuli za Kilimo
    • Shughuli za Ufugaji
    • Shughuli za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha, Mipango & Utawala
      • Elimu, Afya & Maji
      • Mazingira, Ujenzi & Uchumi
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Taratibu Mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za Shughuli Mbalimbali
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERIKALI YAAGIZA KUANZISHWA KWA MADAWATI YA ULINZI WA MTOTO.

Tuma: October 13th, 2017

Na. Samson Chacha Habari leo Tarime.

Serikali imeagiza shule zote za sekondari na msingi, kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule zao ndani ya miezi sita kuanzia sasa ili mtoto akipata shida ajue atakakokwenda kutoa taarifa.

Aidha imezindua kampeni kwa mikoa 10 ya Tanzania Bara, ambayo itahakikisha inatokomeza mimba za utotoni ikihamasisha Watoto wa kike kujilinda, kujithamini na kujipenda ili kufikia matarajio yao.

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema hayo hapa Wilayani Tarime katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.

Katika maadhimisho hayo, wadau mbalimbali wameshiriki katika maandalizi ya siku hiyo ikiwemo Plan International ambapo kauli mbiu ya siku ya mtoto wa kike duniani ni “Tokomeza mimba za utotoni kufikia uchumi wa viwanda”.

Ummy aliagiza kuwa ni lazima shule zote za msingi kuanzisha madawati hayo ya ulinzi na usalama wa mtoto ili mtoto ajue akipata tatizo la ukatili ikiwemo ubakaji, ukeketaji ajue atakimbilia kwa mwalimu yupi au ofisi gani ili atoe taarifa na kupata msaada. Alisema mbali na kuanzishwa madawati hayo pia walimu wakuu wachague mwalimu mmoja au wawili ambao watahakikisha kuhusika katika dawati hilo.

Kuhusu kampeni alisema serikali imezindua kwa mikoa 10 nchini ili kutokomeza mimba za utotoni ambayo itawezesha watoto wa kike kujitambua thamani waliyonayo.

Aliongeza kwa kusema, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zinaeleza kuwa endapo wasichana wakiwezeshwa wanaweza kuchangia katika uchumi kwa asilimia 15 wakati upande wa wanaume ni kwa asilimia 11.

Alisema kampeni ni endelevu ikigusa mikoa hiyo kwa Tanzania Bara ili mtoto wa kike asome kwa bidii huku akisisitiza kuwa serikali ina mpango pia wa kufanya utafiti ili kuwatambua mafataki wanaoharibu malengo ya mtoto wa kike na kuwachukulia hatua.

Aidha alisema mimba za utotoni zina athari kubwa, ambapo asilimia 15 ya vifo vya uzazi vinatokana na watoto kupata ujauzito katika umri mdogo ambapo vifo hutokea kwa wenye umri kati ya miaka 15 hadi 18.

Awali akizungumza, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la watoto Duniani (UNICEF) Maniza Zaman alisema bado tuna kazi ya kufanya katika kuhakikisha mtoto wa kike aliye katika umri wa balehe anavuka kipindi hicho kwa usalama ili kufikia utu uzima. Na kuongeza kuwa ipo haja ya kulelewa kwa watoto wa kike na kiume tofauti na ilivyozoeleka awali.

Matangazo ya Kawaida

  • ORODHA YA VITAMBULISHO VYA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU March 20, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA (DAFTARI LA WAPIGA KURA). April 19, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA February 25, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZIYA MKATABA KWA MADEREVA. May 30, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU 2025

    August 14, 2025
  • WATAALAMU WA MIFUGO WAKABIDHIWA CHANJO ZA KUKU

    July 08, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA UTENDAJI KAZI (ESS) MKOANI MARA

    June 11, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA, SHULE YA SEKONDARI MAGOTO

    June 02, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Maadhimisho ya Nanenane, 2024
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • eMrejesho
  • Dirisha la Watumishi
  • Taarifa za Mishahara
  • NeST-Mfumo wa kielektroni wa manunuzi Tanzania
  • Mfumo wa Usajili Mali iliyopotea
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa wafanyabiashara wadogowadogo
  • Mfumo wa Kibali cha kusafiri nje ya nchi
  • STAFF ASSESSMENT

Viungio Vinavyoshabiana

  • Government portal
  • TAMISEMI
  • HALMASHAURI WILAYA TARIME.BLOG
  • Magazeti mbalimbali
  • Jarida la Tarimedc
  • MWALIMU WETU MITIHANI MBALIMBALI

Idadi ya waliotembelea tovuti kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa