• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Mail za Ofisi |
    • Malalamiko |
TARIME DISTRICT COUNCIL
TARIME DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi na Awali
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Maendeleo ya Jamii,
      • Mipango na Uratibu
    • Kitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Shughuli za Kilimo
    • Shughuli za Ufugaji
    • Shughuli za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha, Mipango & Utawala
      • Elimu, Afya & Maji
      • Mazingira, Ujenzi & Uchumi
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Taratibu Mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za Shughuli Mbalimbali
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WANANCHI KATA YA NYAMWAGA WAPATA ELIMU YA KINYWA NA MENO

Tuma: March 20th, 2018

Wananchi 245 Kata ya Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara wameng’olewa meno kutokana na matatizo ya meno huku Wanafunzi 510 kutoka shule 10 za msingi wakipata Elimu ya Afya ya Kinywa na Meno.

Zoezi hilo limeendeshwa na timu ya Madaktari 21 wa Kinywa na Meno kati ya hao 15 wametoka Dar es Salaam na 6 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kinywa na meno duniani.

Daktari wa Kinywa na meno mkoa wa Mara Dkt Nila Jackson  alisema kuwa Madaktari hao wamegawanyika kimakundi kutoa elimu ya Kinywa na meno mashuleni na katika Vituo vya kutolea huduma ya Afya lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanafahamu namna ya kujikinga pamoja na kuzingatia usafi wa meno.

Wakitoa elimu kwa Wanafunzi wa Darasa la Tatu shule ya msingi Maika Kata ya Nyamwaga Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Dk.David Mapunda aliwataka wanafunzi kutotumia vitu vya sukari kama,Sukari Pipi,Chocolate,Soda kwakuwa vinachangia kuoza na kutoboka kwa meno.

Joseph Kazimoto kutoka Hospital ya Hope Dental iliyoko jijini Mwanza alizitaja baadhi ya dalili za meno ni pamoja na kupata maumivu makali ya jino hasa wakati wa usiku kupata maumivu wakati wa kula na kunywa, huku Lorna Carneiro akiwafundisha kwa vitendo wanafunzi hao jinsi ya kusafisha kinywa na meno kwa kutumia mswaki.

Veronica Marwa Mwanafunzi wa darasa la 3 shule ya msingi Maika alisema hajawahi kupiga mswaki zaidi ya kusukutua mdomo kwa maji nakwamba dawa ya meno na mswaki alivyopewa kama zawadi katika maadhimisho hayo atavitumia ili kinywa na meno kuwa safi.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Muuguzi mkuu kituo cha Afya Nyamwaga Debora Magasi alisema kuwa kufika kwa Madaktari wa meno kituoni hapo wamewawezesha wananchi kupata Elimu na huduma ya meno kwakuwa kituo hicho hakina Daktari wa meno.

Maadhimisho ya wiki ya Afya ya Kinywa na Meno Kitaifa yanafanyika wilayani Tarime ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  “fikiria kinywa fikilia mwili’’

Matangazo ya Kawaida

  • ORODHA YA VITAMBULISHO VYA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU March 20, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA (DAFTARI LA WAPIGA KURA). April 19, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA February 25, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZIYA MKATABA KWA MADEREVA. May 30, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI

    February 20, 2025
  • TANZIA

    March 15, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MARA ATEMBELEA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME

    February 26, 2025
  • MHE. EVANCE MTAMBI AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MWEMA NA RWGICHERI JUU YA CHANGAMOTO YA ARDHI

    February 24, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Maadhimisho ya Nanenane, 2024
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • eMrejesho
  • Dirisha la Watumishi
  • Taarifa za Mishahara
  • NeST-Mfumo wa kielektroni wa manunuzi Tanzania
  • Mfumo wa Usajili Mali iliyopotea
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa wafanyabiashara wadogowadogo
  • Mfumo wa Kibali cha kusafiri nje ya nchi
  • STAFF ASSESSMENT

Viungio Vinavyoshabiana

  • Government portal
  • TAMISEMI
  • HALMASHAURI WILAYA TARIME.BLOG
  • Magazeti mbalimbali
  • Jarida la Tarimedc
  • MWALIMU WETU MITIHANI MBALIMBALI

Idadi ya waliotembelea tovuti kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa