Mheshimiwa Eng. Mtemi Msafiri Mkuu wa wilaya Tarime katika kikao chake na Kamati ya ulinzi na usalama, menajimenti ya halmashauri na wafanyabiashara wa vibanda soko la sirari. Hatimaye wamaliza mgogoro wa umiliki wa vibanda na viwango vya kodi ya kupangisha vibanda hivyo vya halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Katika kikao hicho cha tarehe 17/03/2020 wafanyabiashara kwa pamoja walikiri kwa pamoja kwamba vibanda vya soko la sirari vilivyojengwa na wafanyabiashara mwaka 1998 kwa mkataba wa kipindi cha miaka kumi 10 kwamba vibanda vyote ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Tarime na kuongezwa miaka 10 iliyoishiwa juni 2018/2019.
Hivyo wafanyabiashara waliojenga vibanda au waliopangishwa waanze kutoa kodi ya pango kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020(julai 2019),pia ilisisitizwa kuwa wafanyabiashara wote wasaini mikataba upya ya kupangishwa na halmashauri bila mtu wa katikati kwa kuwa vibanda ni mali ya halmashauri.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa