Katibu Mkuu Tamisemi Mhe. Eng Joseph Nyamhanga katika ziara yake halmashauri ya wilaya ya Tarime ya kutembelea miradi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukagua makao mapya ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime, amewapongeza halmashauri ya wilaya ya Tarime kwa kutii agizo la Mhe DK. John Pombe Joseph Magufuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhamia Nyamwanga na kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi wanyonge,
Katibu Mkuu amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe DK. John Pombe Joseph Magufuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejidhatiti na kuhakikisha kuwa mwananchi wote wanapata huduma iliyobora na kwa urahisi, hivyo serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 za kitanzania kwa halmashauri zaidi ya 30 ambapo zimeagizwa kuhakikisha zinaanza kujenga majengo ya utawala kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi
Aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Tarime kwa kuonesha utayari katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona wakati alipotembelea, kuangalia na kukagua zahanati ya nyamongo iliyotengwa kwa utayari wa kupokea washukiwa wa ugonjwa wa corona endapo atabainika kuwepo mshukiwa. Na kuahidi kuangalia namna ya kuipatia hadhi ya kuwa kituo cha Afya kwa kuwa miundombinu yake katika zahanati hiyo inajitosheleza.
Vilevile akaonesha kufurahishwa na umoja wa viongozi kwa jinsi wanavyofanyakazi kwa pamoja.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa