Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Ndugu Apoo Castro Tindwa akiwakaribisha waseminishaji kutoka chuo cha serikali za mitaa Hombolo, amesema mafunzo haya ni kwajili ya kuwajengea uwezo madiwani wa halmashauri hii hivyo yataboresha uhusiano na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo katika kata zao na halmashauri kwa ujumla.
Mafunzo hayo yaliyogharimiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa muda wa siku mbili - yaliyoanza tarehe 19/01/2021 katika ukumbi wa shule ya sekondari ya JK Nyerere kata ya Nyamwaga, ikiwahusisha waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara. Ikiwa na lengo la kuwajengea madiwani uwezo wa kusimamia uwendeshaji wa halmashauri.
Mada za mafunzo zilizowasilishwa na wataalamu kutoka chuo cha Hombolo ni kuhusu sheria za uendeshaji wa mamlaka za serikali za mitaa, utawala bora na ushirikishaji wananchi, muundo, madaraka na majukumu ya serikali za mitaa.
Mada nyingine ni pamoja na uendeshaji wa vikao na mikutano katika mamlaka za serikali za mitaa, uibuaji, upangaji na usimamizi wa miradi shirikishi katika jamii, usimamizi na uthibiti wa fedha katika mamlaka ya serikali za mitaa.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa