Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amewataka wananchi wote waliovamia maeneo ya Tasisi za Serikali kupisha Mapema ikiwa ni pamoja na kuondoka mara moja Maeneo yalitengwa kwa ajili ya Miundombinu ya Barabara.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri huyo wa Tamisemi kipindi akiongea na wananchi wa kijiji cha Kangariani kata ya Itiryo Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Waitara alisema kuwa Wananchi wamekuwa wakivamia maeneo ya taasisi za kiserikali hivyo sasa amewataka wananchi wote walivamia maeneo hayo kupisha wenyewe kabla ya serikali kuwatoa.
“Wananchi wamevamia sana maeneo hayo ya serikali mpaka mgonjwa hawezi kukimbizwa hospitali kwa sababu ya ufinyo wa barabara, sasa watendaji wa serikali fanyeni kazi ya kupima taasisi za serikali” alisema Waitara.
Pia Waitara alisitiza Viongozi kusimamia vizuri suala la Maendeleo katika ujenzi wa Miundombinu ya Shule za msingi na sekondari na siyo kuingiza suala la Ukabira, itikadi za vyama katika Maendeleo ambapo amechangia kiasi cha shilingi Millioni Moja kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kangariani inayojengwa katika kijiji alichozaliwa.
Wakibainisha Changamoto wananchi wa kijiji cha Kangariani walidai kuwa suala la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ni kubwa pamoja na upatikanaji wa Maji safi na salama.
Apoo Castro Tindwa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Viijijini akijibu hoja za Wananchi mbele ya Naibu waziri alisema kuwa tayari Halmashauri hiyo imetenga Milioni160 kwa ajili ya kukarabati vyumba hivyo vya madarasa ili kupunguza changamoto ya Vyumba vya madarasa
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga alisema kuwa ameamua kuhamasisha Wananchi ili waweze kujenga madarasa wenyewe ili ifikapo Mwezi wa pili wanafunzi watakao chaguliwa kwa awamu ya pili waweze kupata elimu.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa