MKUU wa mkoa wa Mara Ali Hapi ameitaka Halmashauri ya Tarime Dc kutumia mfumo rasmi wa kiserikali katika malipo ya CSR ili kuepusha na kuondokana na ubadhilifu wa fedha za uma na kukwama kwa miradi husika.
“Pesa zote za CSR ni mali ya uma sio za mtu binafsi hivyo utaribu rasmi wa kiserikali ufatwe”.
Aliyasema hayo katika mkutano wa baraza la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa J.K Nyerere Nyamwaga wiki hii.
Pia amekemea tabia ya ubadhilifu wa pesa za uma na kutokamilika kwa miradi kwa wakati kama ujenzi wa wa zahanati ya Nyagisya kata ya Kyore ambapo imebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kupotea kwa kiasi cha Tsh. milioni 70,323,200/= kutoka kwenye akaunti ya kijiji cha Nyagisya na kuitaka Halmashauri kujikita katika mipango ya muda mrefu wa kukamilisha miradi.
“Mkuu wa wilaya, Madiwani, Kamati ya Usalama simamieni utekelezaji wa miradi na pesa za uma na kuwafikisha wote kwenye vyombo vya sheria watakao bainika kufanya uovu maana ndio maelekezo ya serikali”.
Nao madiwani wameendelea kuishukuru serikali na kuaihidi usimamizi bora wa pesa za uma na kuhakikisha miradi inakamilika kwa muda na ubora.
“Tumelipokea vyema swala la pesa kutoka serikali kuu au CSR kwenda moja kwa moja kwenye mradi husika kwenye kata au kijiji maana utapunguza upotevu wa pesa kiholela”. Alisema Amos Sagara diwani wa kata ya Sirari”.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Mara amelipokea ombi la Halmashauri hiyo la matumizi ya Tsh bilioni 7.4 za CSR na kuipongeza Halmashauri ya Tarime DC kwa kuendelea kupokea hati safi mara (6) mfululizo kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka mwaka 2020/2021 na yote kuwa matunda ya Ushirikiano baina ya Wataalamu, Waheshimiwa Madiwani, Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Ofisi ya Mkuu wa mkoa katika kuhakikisha Halmashauri inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa