• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Mail za Ofisi |
    • Malalamiko |
TARIME DISTRICT COUNCIL
TARIME DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi na Awali
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Maendeleo ya Jamii,
      • Mipango na Uratibu
    • Kitengo
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Shughuli za Kilimo
    • Shughuli za Ufugaji
    • Shughuli za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha, Mipango & Utawala
      • Elimu, Afya & Maji
      • Mazingira, Ujenzi & Uchumi
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Taratibu Mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za Shughuli Mbalimbali
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WAKUU WA MIKOA TANZANIA, KENYA WAHAKIKI ALAMA ZINAZOWEKWA ZA KIMATAIFA

Tuma: April 21st, 2018

Imebainika kuwa baadhi ya wananchi wa Tanzania na Kenya wamejenga nyumba pamoja na kufanya shughuli za kilimo katikati ya Mipaka ya Kimataifa inayotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Dk.James Mtambakaya alisema kuwa Wananchi wanatakiwa kusimamisha ujenzi na kutoendeleza maeneo hayo hadi yatakapotolewa maelekezo na Viongozi wa nchi hizo mbili.

“Tanaendelea na uhakiki uboreshaji wa alama za zamani na kuongeza alama zingine mpya ili mwananchi azione kwa urahisi, tunapopita kwenye maeneo kuna watu wamejenga katikati ya mipaka sasa sijui wanajihesabu wako nchi gani” alisema Mtambakaya.

Mtambakaya alisema kuwa zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Umoja wa Afrika (AU) iliyozitaka nchi hizo kupitia na kufanya maboresho ili kuepuka migogoro baina ya nchi hizo mbili nakwamba km 754 za nchi kavu zitahakikiwa na km 56 ni katika ziwa victoria ambapo hadi sasa zimehakikiwa km 25 na kwa awamu ya kwanza zitahakikiwa km 238.

Zoezi hilo la uhakiki limeshuhudiwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima ,Mkuu wa mkoa wa Nyanza Mophat Kangi na Mongo Chimwaga wa Lift Valley (Bonde la Ufa ) nchini Kenya.

Wakuu hao wa Mikoa walitembelea maeneo mbalimbali ya mipaka ya Kimatafa kuangalia alama zilizoboreshwa na alama mpya katika vijiji vya Sirari, Kubiterere, Nyamohonda vilivyopo wilaya ya Tarime na Rorya Vijiji vya Kogaja, Kilongwe.

Nchini Kenya ni vijiji vya Isipania,Kumumwamu,Mti mrabu,Kopanga na Muhuru Kaunti ya Migori ambapo Mkuu wa Mkoa wa Nyanza Mophat Kangi alisema lengo ni kuthibitisha alama hizo nakwamba zoezi hilo ni muhimu kwakuwa wananchi watafahamu mipaka yao na kufanya kazi kwa urahisi.

Mkuu wa Mkoa wa Lift Valley Mongo Chimwaga alisema kuwa baadhi ya wananchi waling’oa alama hizo za zamani zilizowekwa na wakoloni wakijua ndani yake kuna madini na sasa zinaongezwa alama nyingi na kuboreshwa zile za zamani.

“Awali zoezi hili lilifanyika pindi ilipotokea migogoro lakini sasa inafanyika wakati wa amani hatugawi wananchi bali tunataka wajue mipaka ya nchi zao” alisema Chimwaga.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Adamu Malima aliwataka wataalamu wa ardhi wa mipaka kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa kwani isipofanywa vema italeta migogoro huku akihaidi mkoa wa Mara kutoa ushirikiano na timu ya uhakiki lengo kuimarisha mahusano.

Mkaziwa Sab Kaunt ya Kurya West katika Kaunt ya Migori Piter Haiwei alisema kuwa kuwekwa kwa alama hizo itasaidia wananchi kujua mipaka yao ambapo awali waliingiliana katika shuguli za kilimo na ufugaji na kusababisha kutokea kwa migogoro.

Thomas Mwita alisema “Mimi nilinunua ardhi nikapimiwa na watu wa ardhi Migori lakini leo uhakiki mipaka najikuta niko Tanzania nina wake wawili mmoja mji wake umehesabika uko Tanzania na mke wa pili mji wake uko Kenya na mimi ni raia wa Kenya sasa mke wangu nitamweka wapi na sina Ardhi nyingine Kenya”.

Matangazo ya Kawaida

  • ORODHA YA VITAMBULISHO VYA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU March 20, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA (DAFTARI LA WAPIGA KURA). April 19, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA February 25, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZIYA MKATABA KWA MADEREVA. May 30, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • WATAALAMU WA MIFUGO WAKABIDHIWA CHANJO ZA KUKU

    July 08, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA UTENDAJI KAZI (ESS) MKOANI MARA

    June 11, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA, SHULE YA SEKONDARI MAGOTO

    June 02, 2025
  • MAADHIMISHO YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA WATOTO

    June 01, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Maadhimisho ya Nanenane, 2024
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • eMrejesho
  • Dirisha la Watumishi
  • Taarifa za Mishahara
  • NeST-Mfumo wa kielektroni wa manunuzi Tanzania
  • Mfumo wa Usajili Mali iliyopotea
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa wafanyabiashara wadogowadogo
  • Mfumo wa Kibali cha kusafiri nje ya nchi
  • STAFF ASSESSMENT

Viungio Vinavyoshabiana

  • Government portal
  • TAMISEMI
  • HALMASHAURI WILAYA TARIME.BLOG
  • Magazeti mbalimbali
  • Jarida la Tarimedc
  • MWALIMU WETU MITIHANI MBALIMBALI

Idadi ya waliotembelea tovuti kidunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa